Mjamzito na mnyonyeshaji wanapaswa kulipa peke yake?

Swali: Miaka miwili ya nyuma mwezi wa Ramadhaan nilikuwa mgonjwa na sikuweza kufunga siku saba. Baada ya hapo nikasimama na nikalisha kwa kila siku moja masikini. Je, inatosha kufanya hivo? Je, ni lazima kwangu kulipa siku hizo?

Jibu: Ndio, ni lazima kwako kulipa pamoja na kulisha. Ikiwa ulikula kwa sababu ya mimba basi yanakulazimu mambo mawili; kulipa na kulisha. Tayari umeshalisha na kilichobaki ni kulipa. Ama ikiwa ulikula kwa sababu ya afya yako wewe, basi kitachokulazimu ni kulipa peke yake pasi na kulisha.

Kusema kwamba jambo la kulipa linadondoka – kama ulivyotaja – si sahihi. Ni madhehebu yenye kurudishwa ingawa yamepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas na Ibn ´Umar. Ni maoni yasiyokuwa na nguvu. Ni lazima kwa mwenye mimba na kwa mwenye kunyonyesha wakila basi walipe kwa hali zote. Kuhusu kulipa ndio jambo linalohitajia upambanuzi. Ikiwa ulikula kwa sababu ya mimba peke yake, basi utatakiwa kulipa na kulisha maskini kwa kila siku moja uliyokula. Ama ikiwa ulikula kwa sababu ya afya za kiujauzito, basi atatakiwa kulipa peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (1-2)
  • Imechapishwa: 06/09/2019