Mjamzito anayetokwa na mkojo kila wakati kuacha kuswali

Swali: Mwanamke mjamzito anasumbuliwa kutokwatokwa na mkojo kila wakati. Nilisimamisha kuswali katika mwezi wa mwisho. Je, huku ni kuacha swalah na ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Haifai kwa mwanamke aliyetajwa na mfano wake kusimamisha swalah. Bali ni lazima kwake kuswali kutegemea na hali yake na atawadhe wakati wa kila swalah kama mfano wa mwanamke mwenye damu ya ugonjwa. Anatakiwa kujihifadhi kwa kile anachoweza katika pamba na vyenginevyo na aswali ndani ya wakati wake. Inakubalika katika Shari´ah kwake yeye kuswali swalah zilizopendekezwa katika wakati wake. Inafaa kwake kujumuisha kati ya swalah mbili Dhuhr na ´Aswr, Magrhib na ´Ishaa kama mfano wa mwanamke mwenye damu ya ugonjwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

اتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Ni lazima kwake kulipa zile swalah alizoacha pamoja na kutubia kwa Allaah kwa njia ya yeye kujutia yale aliyoyafanya na aazimie kutorudia kufanya hivo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Tubuni kwa Allaah nyote, enyi waumini, mpate kufaulu.”[2]

[1] 64:16

[2] 24:31

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/224)
  • Imechapishwa: 06/09/2021