Mjamzito ameacha swalah kwa kushindwa kuinuka kutoka kitandani

Swali: Mke wangu alikuwa mjamzito ambaye anatokwa na maji mengi ya fetasi ambapo akaingia hospitalini kuanzia saa kumi alfajiri hadi saa kumi na moja jioni. Daktari akamzuia kuinuka kutoka kitandani na hakuswali siku hiyo. Ni ipi hukumu?

Jibu: Kinachopasa ni yeye kuswali vile alivyo, hata kama itakuwa juu ya kitanda. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kumwambia mgonjwa:

“Swali kwa kusimama. Usipoweza, kwa kukaa. Usipoweza, kwa ubavu.”

Kwa hivyo ingelikuwa vyema endapo mume angemwelekeza kufanya hivo. Ikiwa mambo yameshakuwa hivo na uhalisia wa mambo ni kama ilivyotajwa, basi azirudie swalah zake ambazo aliacha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/من-نزل-منها-ماء-الجنين-قبل-صلاة-الظهر
  • Imechapishwa: 12/06/2022