Mja kulindwa na Allaah kutofanya maovu

Swali: Ni ipi tafsiri sahihi ya Hadiyth al-Qudsiy Swahiyh inayosema:

“Akinijia hali ya kutembea basi nitamwendea hali ya kuchepua?”

Jibu: Yanafasiriwa kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Akiniomba Nitampa na akiniomba ulinzi Nitamlinda.”[1]

Maana yake ni kwamba Allaah ataharakia haja yake na humtia nguvu kwa mikono yake atayoshika kwayo na miguu yake atayotembea kwayo. Kwa msemo mwingine ni kwamba Atalinda viungo hivi kutofanya maovu. Atakuwa na pamoja Naye upamoja maalum ambao maana yake ni kutiwa nguvu, kunusuriwa na kujaaliwa.

[1] al-Bukhaariy (6502).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 46
  • Imechapishwa: 09/06/2021