Swali: Ni mizani ipi inayopima kati ya Bid´ah na Sunnah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyataja hayo kwa mizani adilifu. Amesema:

“Hakika Ummah huu utagawanyika katika mapote sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakauliza: “Ni lipi hilo, ee Mtume wa Allaah ?” Akasema: “Ni wale wataokuwa juu ya yale niliyokuwemo mimi na Maswahabah zangu.”

Hii ndio Sunnah. Yule ambaye atakuwa ni mwenye kufuata nyayo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawa anafuata mwenendo wake katika ´Aqiydah, maneno na vitendo vyake, basi huyu ndiye aliye katika Sunnah. Yule mwenye kwenda kinyume hayuko katika Sunnah. Lakini haifai kupinga ya kwamba hayuko katika Sunnah upingaji wa moja kwa moja. Bali tunatakiwa kusema kuwa ni mwenye kwenda kinyume na Sunnah katika jambo hili pekee. Kwa sababu tunatakiwa kutambua tofauti kati ya kusema kwa kuachia na kwa kufungamanisha. Hatuna haki pindi tunapomuona mzushi kusema kuwa ni katika Ahl-ul-Bid´ah. Bali tunatakiwa kufungamanisha ya kwamba ni katika Ahl-ul-Bid´ah katika jambo fulani. Kwa sababu mtu anaweza kuwa amezua jambo. Lakini hata hivyo akawa ni mwenye kushikamana na Sunnah katika mambo mengi. Huyu si sawa kumpachika ya kwamba ni mzushi. Bali mtu anatakiwa kusema kwa kufungamanisha. Hii ndio mizani adilifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/907
  • Imechapishwa: 08/09/2018