Swali: Mizani siku ya Qiyaamah ni ya kihisia au ni ya kimaana?

Jibu: Hapana, ni ya kihisia. Ni mizani ilio na vitanga viwili na ulimi. Ni mizani ya kihisia. Wanaosema kuwa ni mizani ya kimaana ni Mu´tazilah na wapotevu. Hawa ndio wanasema kuwa ni mizani ya kimaana. Kuhusiana na Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa ni mizani ya kihakika ilio na vitanga viwili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (78) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/taf_3_1_1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020