Mitume wamekingwa katika wanayofikisha

Swali: Je, Mitume wamelindwa kwa madhambi yote?

Jibu: Mitume wamekingwa kwa yale wanayofikisha kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa), bi maana katika kufikisha ujumbe, madhambi makubwa na kuendelea na dhambi ndogo. Mmoja wao akitumbukia kwenye dhambi ndogo anakimbilia kufanya Tawbah kwa kuwa Allaah Hakutaja kitu kutoka kwa Mtume yeyote isipokuwa ameambatanisha hilo kwa Tawbah kuwa ametubu kwa jambo hilo mwishoni. Ama kuhusu kufikisha ujumbe na madhambi makubwa wamekingwa kuanzia mwanzoni na mwishoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 09/08/2020