Swali: Je, inajuzu kwa mtu kula katika Ramadhaan kwa sababu ya masomo?

Jibu: Haifai kwa wanafunzi kula katika Ramadhaan kwa sababu ya mitihani. Bali ni lazima kwao wajitahidi na wafanye maandalizi usiku kwa ajili ya mitihani yao na mchana wafunge. Vivyo hivyo kwa wafanya kazi haifai kwao kula. Bali ni lazima kwa mfanya kazi afanye kazi kwa kiasi cha uwezo wake mchana wa funga. Kadhalika wanafunzi wafanye kazi kwa yale yanayohusiana na mitihani kwa kiasi cha uwezo wao wakati wa mchana. Watilie umuhimu kufanya mazoezi wakati wa usiku. Kwani hilo ndio lenye nguvu zaidi kwao. Wale wahusika wawafanyie wepesi mchana na wasiwafanyie ukali kwa hilo mpaka wakawatia uzito kwa swawm zao. Yakiwezekana hayo kufanyika kabla ya Ramadhaan au baada ya Ramadhaan ndio bora zaidi ili wasiwatie uzito wanafunzi. Lakini mitihani na kazi sio udhuru wa kutokufunga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/6892/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%81%D8%B7%D8%A7%D8%B1-%D8%B1%D9%85%D8%B6%D8%A7%D9%86-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D8%AC%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%85%D8%AA%D8%AD%D8%A7%D9%86%D8%A7%D8%AA-%D8%A7%D9%84%D8%AF%D8%B1%D8%A7%D8%B3%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 27/04/2020