Misingi mine kwa Raafidhwah

Misingi ya dini ya Raafidhwah ni mine:

  1. Tawhiyd.
  2. Uadilifu.
  3. Utume.
  4. Uimamu.

Uimamu ndio daraja ya mwisho na Tawhiyd, uadilifu na utume ni kabla yake.

Wanaingiza ndani ya Tawhiyd kukanusha sifa za Allaah, kwamba Qur-aan imeumbwa na kusema kwamba Allaah hatoonekana Aakhirah.

Wanaingia ndani ya Uadilifu kukadhibisha Qadar na kwamba Allaah hawezi kumwongoza amtakaye, kwamba hawezi kumpoteza amtakaye, kwamba Anaweza kutaka kitu na kisiwe, kwamba kukawa kitu Asichokitaka na mengineyo. Hawasemi kuwa Allaah ndiye muumba wa kila kitu au kwamba ni muweza juu ya kila kitu. Hawasemi kwamba Anachotaka Allaah, basi kinakuwa, na kwamba Asichokitaka, basi hakiwi.

Ni vipi Uimamu utakuwa ni kitu kitukufu na muhimu zaidi kwao ilihali wametanguliza Tawhiyd, Uadilifu na utume kwanza?

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/99)
  • Imechapishwa: 29/01/2019