Swali: Unasemaje juu ya kuharakisha kutoa zakaah kwa wanyonge walioko Chechenia?

Jibu: Sioni ubaya kufanya hivo. Naona kuwa Chechenia hivi sasa wanahitajia zakaah; wapambanaji katika njia ya Allaah na wakimbizi katika mafukara na masikini. Nawahimiza ndugu zangu kuwasaidia. Ni mamoja ikiwa ni zakaah au swadaqah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1605