Swali: Baba yangu amefariki na ameacha kiwanja. Bora zaidi ni kuigawa au iuzwe na kumwacha mtu mwengine amhijie kwa pesa hizo?

Jibu: Ikiwa hakuhiji hapo kabla basi ahijiwe kabla ya mirathi kugawiwa. Ni katika haki ambazo ziko juu ya dhamiri yake na hivyo inatakiwa kutangulizwa. Mambo ni hivyo ikiwa hakuwahi kuhiji hapo kabla. Chenye kubaki baada ya hajj watagawiwa warithi. Lakini ikiwa lengo ni hajj ya Sunnah, gharama zake zisichukuliwe kutoka katika mirathi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20-%2024-10-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017