Miongoni mwa sababu zinazotumbukiza katika Bid´ah

4- Kujifananisha na makafiri. Ni miongoni mwa vitu khatari vinavyotumbukiza katika Bid´ah kama ilivyo katika Hadiyth ya Abu Waaqid al-Laythiy amesema:

“Tulitoka pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuelekea Hunayn na sisi ndio bado karibuni tulikuwa tumetoka katika ukafiri. Washirikina walikuwa na mkunazi wakikaa hapo kwa muda mrefu na wakitundika silaha zao juu ambao ulikuwa ukiitwa Dhaat an-Waatw. Tukapita kwenye mti mwengine wa mkunazi tukasema: “Ee Mtume wa Allaah! Tufanyie na sisi Dhaat an-Waatw kama ambavyo wao wako na Dhaat an-Waatw?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaahu ni mkubwa! Ndio zilezile njia [za makafiri]. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, kwa hakika mmesema kama walivosema wana wa israaiyl kumwambia Muusa:

اجْعَل لَّنَا إِلَهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ

“Tufanyie mungu kama ambavyo wao wako na miungu!” Akasema: “Hakika nyinyi ni watu wajinga!”[1]

Hakika mtafuata njia za wale waliokuwa kabla yenu.”[2]

Katika Hadiyth hii imepata kufahamika kwamba kujifananisha na makafiri ndio jambo lililowafanya wana wa israaiyl kutaka maombi haya mabaya; wafanyiwe mungu wa kumwabudu. Vilevile ndio jambo lililowafanya Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuomba awafanyie mti ambao watakuwa wanafanya Tabarruk kwao badala ya Allaah. Hali ndio hiyohiyo hii leo. Watu wengi katika waislamu wamejifananisha na makafiri katika Bid´ah na mambo ya shirki. Kama mfano wa sherehe ya maulidi, kufanya masiku na mawiki kwa ajili ya matendo maalum, kusherehekea minasaba ya kidini na ya ukumbusho, kufanya masanamu, masanamu ya ukumbusho, kufanya matanga, Bid´ah za mazishi, kuyajengea makaburi na nyenginezo.

[1] 07:138

[2] Ahmad (21947) na tamko ni lake na at-Tirmidhiy (2185).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 187-188
  • Imechapishwa: 21/11/2019