Miongoni mwa adabu za du´aa


Swali: Leo maimamu wamekithirisha kufanya du´aa. Tunaomba kuelezwa adabu za du´aa na makatazo yake.

Jibu: Maimamu na waswaliji wanajiombea wenyewe wanapokuwa katika Sujuud, Tashahhud na baina ya sijda mbili. Lakini kuhusu du´aa inayowahusu watu wote, kama mfano wa du´aa ya Qunuut, mtu anatakiwa kwanza ahifadhi yale mambo yaliyothibiti. Kwa sababu du´aa zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zote ni kheri. Du´aa hizo zina kheri nyingi kabisa kuliko baadhi ya du´aa zenye mashaji´isho ambazo zimetengezwa na watengenezaji. Du´aa zilizopokelewa ndio zenye kheri zaidi. Halafu hakuna neno iwapo atazidisha juu yake. Lakini hata hivyo achunge vile wanavyoonelea wengi katika wale walioko nyuma. Kwa sababu wapo watu ambao wanapenda kurefusha sana na upande mwingine wapo wanaopenda kufupisha sana. Mtu anatakiwa kufanya kati na kati. Zikiwepo hali ambazo zinapeleka kufupisha basi mtu afanye hivo. Kwa mfano hali ya hewa ni yenye baridi sana na watu wanataka kutekeleza haja kubwa na ndogo. Katika hali hii anatakiwa kutazama hali ya wale wanyonge. Kadhalika hali ya hewa ikiwa ni yenye joto kali anatakiwa vilevile kutazama hali hii. Lakini hata hivyo hali ya hewa ikiwa ni ya kati na kati ndio vizuri na hivyo anatakiwa kufanya kait na kati; asirefushe kunakopelekea kuchoka na wala asifupishe kunakopelekea kuharibu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1588
  • Imechapishwa: 17/10/2018