Swali 1216: Ni ipi hukumu ya kusalimiana na wanawake kwa kupeana nao mikono?

Jibu: Kupeana mikono na wanawake ni jambo linahitajia maelezo. Ikiwa wanawake hao ni katika Mahram zake kama mama yake, msichana wake, dada yake, shangazi yake, mama yake mdogo na mkubwa na mke wake hakuna neno. Ikiwa si katika Mahram zake haijuzu. Mwanamke alimpa mkono Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema:

“Mimi sipeani mikono na wanawake.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Ninaapa kwa Allaah kwamba mkono wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haukuwahi hata siku moja kugusa mkono wa mwanamke. Alikuwa akiwapa bay´ah kwa maneno.”

Haijuzu kwa mwanamke kupeana mkono na mwanaume asiyekuwa Mahram yake. Kadhalika haijuzu kwa mwanaume kupeana mkono na mwanamke asiyekuwa Mahram yake kutokana na Hadiyth mbili zilizotajwa. Jengine ni kwa sababu kitendo hicho hakuaminiwi juu yake ftina.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 489
  • Imechapishwa: 12/08/2019