Mimi naonelea kuwa ni kafiri…


Swali: Kuna ambao wanalingania katika umoja wa dini na wanadai ya kwamba waislamu, mayahudi na manaswara ni wenye kuafikiana katika ule msingi wa dini. Je, mtu kama huyu ahukumiwe ukafiri? Unasemaje juu ya hili?

Jibu: Mimi naonelea kuwa mtu huyu ni kafiri. Yule anayesema kuwa dini ya Uislamu, uyahudi na unaswara ni kafiri kwa sababu anamkadhibisha Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa anaonelea kuwa manaswara, wale ambao wana imani ya utatu, ya kwamba ni wenye kumuabudu Allaah peke yake, basi mtu huyu sio mpwekeshaji. Kwa sababu ameridhia ukafiri na shirki. Ni vipi wale wenye kusema ´Iysaa ni mwana wa Allaah na kwamba ´Uzayr ni mwana wa Allaah watakuwa na umoja na wale wenye kusema:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌاللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

”Sema: “Yeye ni Allaah Mmoja pekee. Allaah ambaye ni mkusudiwa wa yote. Hakuzaa na wala hakuzaliwa. Na wala hakuna yeyote anayelingana Naye.””[1]

Kwa ajili hii mimi namwambia mtu huyu atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).  Huku ni kuritadi ambako kunafanya damu na mali ya mtu kuwa ni halali. Vilevile kunafanya ndoa ya mtu huyu kuvunjika. Isitoshe akifa hastahiki kupewa heshima yoyote. Bali anatakiwa kutupwa kwenye shimo ili watu wasiudhike na harufu yake mbaya. Si halali kwa yeyote kukuombea msamaha ikiwa utakufa katika hali kama hii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake. Hakuna yeyote kutoka katika Ummah huu atasikia kuhusu mimi, sawa awe myahudi au mnaswara, halafu asiamini – au alisema: ”… halafu asifuate yale niliyokuja nayo isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.”

Dini za kimbingu zinabaki ni dini midhali hazijafutwa. Zinapofutwa basi hazizingatiwi kuwa ni dini tena. Mayahudi wakati Shari´ah ya Muusa ilikuwa ni yenye kufanya kazi na wakati huohuo ni wenye kumfuata walikuwa ni wenye kuzingatiwa waislamu. Kadhalika manaswara wakati Shari´ah ya ´Iysaa ilikuwa ni yenye kufanya kazi na wakati huohuo ni wenye kumfuata walikuwa ni wenye kuzingatiwa waislamu. Lakini baada ya kutumwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wote ni wenye kuzingatiwa makafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

”Yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]

[1] 112:01-04

[2] 03:85

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (30) http://binothaimeen.net/content/676
  • Imechapishwa: 10/10/2017