Mimba kupomoroka baada ya miezi miwili

Swali: Mwanamke mimba yake imeporomoka miezi miwili baadaye. Je, aswali na afunge kwa kuzingatia ya kwamba anatokwa na damu?

Jibu: Kama mimba yake iliporomoka baada ya siku 81, basi asiswali na wala asifunge. Ama kama mimba yake iliporomoka chini ya siku 81, afunge na aswali. Kabla ya siku 81 ni damu tu na wala haimzuii mtu kutokamana na kufunga na kuswali. Damu inayotoka baada ya siku 81 inamzuia kutokamana na kuswali na kufunga kwa sababu inaingia katika awamu ya tatu ya siku arobaini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (19) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-22011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 02/12/2019