460- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Siku ya Qiyaamah Allaah hatomwangalia yule mtu ambaye anaiburuta nguo yake kwa kiburi.” Umm Salamah: ”Wanawake wafanye nini na mikia yao?” Akasema: ”Waburute shibiri moja.” Akasema: ”Basi nyayo zao (miguu yao) itaonekana.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Basi waburute dhiraa moja.”

Ameipokea Abu Ya´laa katika ”al-Musnad”[1].

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Wapokezi wake ni waaminifu na ni wanaume wa al-Bukhaariy na Muslim isipokuwa tu Ibraahiym bin al-Hajjaaj ambaye ni mwaminifu.

Katika Hadiyth kuna dalili inayoonyesha kuwa unyayo wa mwanamke ni ´Awrah, jambo ambalo lilikuwa linatambulika kwa wanawake wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaambia: ”Waburute shibiri moja.” Umm Salamah akasema: ”Basi nyayo zao (miguu yao) itaonekana.” Ni jambo linaloashiria kwamba alikuwa akitambua kuwa nyayo za mwanamke ni ´Awrah na hazijuzu kuonekana. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha aburute urefu wa dhiraa moja. Qur-aan tukufu imeashiria hilo pale Allaah (Ta´ala) aliposema:

وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ

“Wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao.”[2]

[1] 1/325.

[2] 24:31

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/2/827-828)
  • Imechapishwa: 19/05/2019