Migahawa inayochoma nyama ya ng´ombe na ya nguruwe sehemu moja

Swali: Baadhi ya migahawa Ulaya wanauza nyama ya ng´ombe na ya nguruwe za kuchomwa na zote zinachomwa kwenye chombo kimoja lakini hata hivyo hazichanganywi. Imesemekana kuwa kitendo hicho kinajuzu kwa kuwa moto unasafisha. Je, ni sahihi?

Jibu: Hapana. Si sahihi. Jambo hili linahitajia kuangaliwa. Inachomwa pamoja na nyama ya nguruwe? Si sahihi. Inanajisika kwa nyama ya nguruwe. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema kuhusu nguruwe:

أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ

“… au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni chafu.” (06:145)

Nyama ya nguruwe ni najisi. Haitwahariki kwa kupikwa wala kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017