Michezo ya watoto ya viumbe vyenye roho ni haramu

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia michezo ya viumbe vyenye roho vinavyokuwa majumbani kwa aina ya wanyama kama ngamia au mtu?

Jibu: Haijuzu. Haya ni masanamu. Haijuzu kuwalea watoto wenu juu ya mapicha na masanamu. Kuna michezo isiyokuwa picha. Kuna michezo mingi mbali na picha kama mfano wa gari, silaha au vitu vyengine mbali na mapicha ya viumbe vilivyo na roho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 02/12/2017