Swali: Inajuzu kukaa na kuzungumza mambo ya kidunia na kucheza msikitini? Baadhi ya watu wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaacha wahabeshi wacheze msikitini.

Jibu: Mchezo huu sio ambao wewe unamaanisha, nao ni mchezo wa upuuzi. Mchezo wa wahabeshi ulikuwa wa mikuki, wanafanya mazoezi namna ya kutumia salaha. Mkuki ni silaha. Inajuzu kufanya mazoezi namna ya kutumia silaha hata kama itakuwa ndani ya msikiti. Hakuna neno, ni katika njia za Jihaad. Hata hivyo haijuzu kucheza msikitini ikiwa michezo hiyo haisilihi Jihaad. Misikiti haikujengwa kwa sababu hiyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (6) http://alfawzan.af.org.sa/node/14379
  • Imechapishwa: 01/12/2016