Swali: Ni ipi bora masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan au masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah?

Jibu: Masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan ni bora inapokuja katika masiku yake. Kwa sababu ndani yake upo usiku wa Qadr ambao ndio usiku bora kabisa. Masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah ni bora inapokuja katika michana yake. Kwa sababu ndani yake ipo siku ya ´Arafah na siku ya kuchinja ambayo ndio michana miwili bora zaidi ulimwengu.  Haya ndio yenye kutegemewa kwa wale wanazuoni wahakiki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/8908/الافضلية-بين-العشر-الاواخر-من-رمضان-وعشر-ذي-الحجة
  • Imechapishwa: 07/07/2021