Miaka yote hii gerezani – faida iko wapi?


Mcheni Allaah juu ya Ummah! Mcheni Allaah juu ya nafsi zenu! Mcheni Allaah juu ya Ummah huu na juu ya mabarabaro wa waislamu. Wafunzeni yale yenye kuwanufaisha. Wafunzeni Qur-aan na Sunnah. Hivi sasa wamekaa wamefungwa kwenye kisiwa cha Khawaarij Guantanamo. Huko mmoja wao anasema: “Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab alinishauri. Allaah amjaze kheri. Ola wangu lau ningekubali ushauri wake.” Mpaka hivi sasa yuko huko. Anajuta kwa vile hakupokea nasaha zangu. Ni mambo ni namna hiyo. Sijui kakaa huko jela miaka mingapi sasa. Faida iko wapi ya mambo haya? Enyi vijana! Fuateni mwongozo! Enyi vijana! Kuwa na akili! Enyi vijana! Jifunzeni dini! Huenda mmoja wao anasema mpaka lini? Baada ya hapo Allaah tu ndiye anayejua atashika njia ya kwenda wapi. Uwezekano mkubwa ni wa yeye kuuliwa. Fuatani mwongozo, tafuteni elimu, jifunzeni dini na fanyeni ya usawa. Elimu haimfanyi mtu akawa na fujo na matatizo. Ninawanasihi wazazi wakitilia umuhimu juu ya wana na vijana wao. Enyi ndugu! Nyinyi ndio malengo. Mabarobaro kutoka Misri, Yemen, Sudan, Saudi Arabia na miji mingineyo wameshika njia wameenda. Masikini, wamesafishwa vichwa na watu walio na mifumo ya kupinda.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ath-Thabaat ´alaa as-Swiraat al-Mustaqiym yakuun bil-´Ilm http://olamayemen.com/Dars-9998
  • Imechapishwa: 06/05/2018