Mgonjwa wa miaka mingi Ramadhaan atoe chakula au asubiri mpaka atapopona?

Swali: Kuna mwanamke ni mgonjwa na madaktari wamemuandikia dawa ambazo anatakiwa kutumia kila siku ndani ya masaa 24 kwa muda mwa miaka mitano, baada ya hapo huenda akapona na huenda asipone. Afanye nini katika mwezi wa Ramadhaan kwenye miaka hii mitano; alishe au asubiri mpaka apone ndio alipe?

Jibu: Ramadhaan aache kufunga na atumie dawa. Akipona baada ya hapo alipe, na madaktari wakimthibitishia kuwa kupona kwake hakutarajiwi, hapo ndipo atatakiwa kulisha. Ikishindikana kulipa, hapo ndipo atatakiwa kulipa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14759
  • Imechapishwa: 28/06/2020