Mgonjwa wa maradhi sugu amepona baada ya Ramadhaan


Swali: Madaktari wamethibitisha kuwa mgonjwa fulani maradhi yake si yenye kutarajiwa kupona ambapo akaacha kufunga. Baada ya muda Allaah akamponya. Je, ni lazima kwake kulipa?

Jibu: Akiwa aliwahi kutoa chakula, hahitajii kufanya kitu zaidi. Ama ikiwa alikuwa bado hajalisha chakula na anaweza kulipa masiku hayo, afanye hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (18) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-15011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2019