Mgonjwa ameswali kwa kukusanya na kufupisha


Swali: Niliswali kwa kukusanya na kufupisha kati ya Dhuhr na ´Aswr hospitalini. Niliuliza nikaambiwa inafaa kwangu kukusanya na kufupisha. Je, ni wajibu kwangu kuzirudi swalah nilizoswali katika kipindi hichi?

Jibu: Swali hili linahitajia ufafanuzi. Ikiwa hospitali hiyo iko katika mji wake basi ni wajibu kwake kurudi zile swalah zote alizoswali hali ya kufupisha. Ikiwa hospitali hiyo iko katika mji/nchi nyingine, basi kitendo chake ni cha sawa na wala hana dhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/730
  • Imechapishwa: 25/11/2017