Mgonjwa amenuia kulipa madeni yake akafa baada ya Ramadhaan

Swali: Kuna mtu aliyefariki siku ya ´Iyd-ul-Fitwr ambapo maradhi yalimpata siku ya kwanza au ya pili ya Ramadhaan ikampitia yote hali ya kuwa ni mwenye kula. Je, ni wajibu kwa warithi wake kumfungia baada ya kufa kwake au ni wajibu kwao kumtolea chakula au hakuna kinachomlazimu yule maiti wala warithi wake?

Jibu: Ikiwa maradhi haya alikula kwa kutokuweza kwake kufunga na akawa hakuweza kulipa kwa sababu alikufa siku ya ´iyd, basi itakuwa sio wajibu kwake kwa kutokuweza kwake kwa sababu ya maradhi yake. Haimuwajibikii kwake kulipa kwa sababu ya kutokuweza kwake kufunga kwa kuwa alikufa siku ya ´iyd. Sio lazima kwa warithi wake kumfugia wala kumtolea chakula.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/370)
  • Imechapishwa: 23/06/2017