Mgonjwa amekufa baada ya Ramadhaan akiwa na deni la Ramadhaan

Swali: Tarehe 21 Ramadhaan iliyopita baba yangu alikula kwa sababu ya maradhi na akafariki hospitalini tarehe 9 Shawwaal. Ni ipi hukumu?

Jibu: Ikiwa alikuwa na maradhi yasiyotarajiwa kupona basi anatakiwa kutolewa chakula kwa kila siku moja kumlisha masikini. Na ikiwa ni maradhi yanayotarajiwa kupona lakini baada ya Ramadhaan kwisha maradhi yakamzidi – kama lilivyo swali lako – mpaka akafariki basi hakuna kinachomlazimu. Kwa sababu ilikuwa ni wajibu kwake kulipa. Lakini hakuweza kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/122)
  • Imechapishwa: 19/06/2017