Mgonjwa amekufa akidaiwa siku kumi za Ramadhaan


Swali: Kuna mwanamke mgonjwa ambaye madaktari wamethibitisha ya kwamba asifunge kwa sababu inamdhuru. Lakini hata hivyo akajipa jukumu la kufunga siku ishirini katika Ramadhaan iliyopita. Mwanamke huyo amefariki mwezi mmoja uliyopita na wala hakukamilisha zile siku kumi zilizokuwa zimebaki. Ni lipi la wajibu juu ya siku kumi zilizobaki? Afungiwe au alishiziwe?

Jibu: Lililo la wajibu ni kulishiziwa masikini mmoja kwa kila siku moja alioacha. Kwa sababu mwanamke huyu – kama inavyodhihiri katika swali – ni mwenye kutoweza kufunga kutokuweza ambako hakutarajii kuondoka. Mtu ambaye hawezi kufunga kutokuweza ambako hakutarajii kuondoka ni wajibu kwake kutolewa chakula. Kwa hivyo lililo la wajibu kwao ni wao kumtolea chakula mwanamke huyu kuwalisha masikini kumi kwa sababu kulikuwa kumebaki siku kumi. Ni wajibu kwao kuwalishiza masikini kumi. Inakuwa vipi? Ima wanaweza kuwaalika masikini kumi katika chakula cha mchana au cha jioni au wampe kila masikini takriban 1 kg. Zote kwa jumla inakuwa takriban 10 kg. Si vibaya pia kuiambatanisha na nyama kidogo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (31) http://binothaimeen.net/content/706
  • Imechapishwa: 13/05/2018