Mgonjwa amefanya Tayammum pamoja na kuwa na uwezo wa kutawadha

Swali: Baba yangu alifanyiwa upasuaji na alikuwa anaweza kuyaendea maji. Lakini alikuwa akifanya Tayammum na akikusanya swalah kwa muda wa karibu siku tatu. Ni kipi kinachomlazimu kwa kuzingatia kwamba ni mjinga alikuwa hajui kitu hicho akidhania kuwa inafaa? Tunaomba maelekezo pamoja na kumnasihi juu ya hili kwa ajili ya kufungua moyo wake na kumpendeza juu ya kheri.

Jibu: Naona kuwa ni wajibu kwa huyu afanye tena. Maadamu alikuwa hospitalini ambapo kuna katika mazingira hayo wapo ambao wanajua haki. Yuko na wanafunzi na yuko na simu. Alitakiwa kuuliza. Kwani yuko katika hali ambayo inapelekea kuuliza kwa sababu ni mgonjwa. Alitakiwa kuuliza ni vipi atajisafisha na ni vipi ataswali; aelekee Qiblah au hapana, asimame au hapana na mfano wa maswali kama hayo. Amezembea. Naona kuwa anatakiwa kulipa zile swalah alizoswali pasi na kuwa na wudhuu´. Katika hali hii ikiwa zile swalah za alizoswali zilikuwa  ni sahihi basi hizi za mwisho zitageuka kuwa Sunnah. Ikiwa zile swalah za alizoswali hazikusihi basi hizi swalah za mara ya pili zitakuwa ni faradhi na zile za kwanza zitakuwa ni Sunnah. Kwa vovyote Allaah atamlipa kwa kiasi cha matendo yake japokuwa alikosea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (51) http://binothaimeen.net/content/1159
  • Imechapishwa: 29/06/2019