Swali: Ni kipi kinachomlazimu mgonjwa aliyekula Ramadhaan?

Jibu: Allaah amejibu jambo hili ndani ya Qur-aan:

فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

”Yule atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au akawa safarini, basi akamilishe idadi katika masiku mengineyo.” (02:184)

Ikiwa ni maradhi ya kujitokeza ghafla na yakaondoka, basi ni lazima kulipa siku ulizokula kabla ya kuingia Ramadhaan nyingine. Akichelewesha mpaka kukaingia Ramadhaan nyingine ni lazima kwake vilevile kulisha? Maoni sahihi kwa mtazamo wangu ni kwamba hakua kinachomlazimu isipokuwa tu kulipa zile siku anazodaiwa kwa mujibu wa Aayah:

فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

”Yule atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au akawa safarini, basi akamilishe idadi katika masiku mengineyo.” (02:184)

Si lazima kwake kutoa chakula.

Lakini maradhi yakiwa ni yale yasiyotarajiwa kupona basi anatakiwa kumlisha masikini kwa kila siku moja ambayo hakufunga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/372)
  • Imechapishwa: 24/05/2019