Mgonjwa aliyelazwa kwenye koma (ICU) na Ramadhaan


Swali: Kuna mwanamke alilazwa kwenye koma mwanzoni mwa Ramadhaan mpaka sasa bado yuko kwenye koma. Ni wajibu kumlishizia au swawm kwake imeanguka au tufanye nini?

Jibu: Mwanamke huyu ambaye amelazwa kwenye koma ikiwa kuna matarajio na yeye kuamka basi kusubiriwe mpaka aamke. Ama ikiwa hakuna matarajio ya yeye kuamka basi alishiziwe kwa kila siku moja masikini mmoja. Ikiwa hakuna matarajio ya yeye kuamka anaingia katika jumla ya wagonjwa na anakuwa ni mwenye maradhi ambayo hayatarajiwi kwake kupona. Mgonjwa mwenye maradhi yasiyotarajiwa kupona anatolewa chakula kwa kila siku moja masikini. Lakini ikiwa kuna matarajio ya yeye kuamka na kupata afya basi wasubiri mpaka aamke. Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1598
  • Imechapishwa: 30/05/2018