Mgonjwa aliyefariki katika Ramadhaan akiwa na deni

Swali: Mamangu alikuwa mgonjwa siku sita kabla ya Ramadhaan. Baada ya siku tano za Ramadhaan akafariki. Je, swawm ni wajibu kwake?

Jibu: Ikiwa maradhi yake sio yenye kutarajiwa kupona basi anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini. Kwa sababu kila mtu ambaye anajiwa na Ramadhaan ilihali yuko na maradhi ambayo hayatarajiwi kupona anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/116)
  • Imechapishwa: 07/06/2017