Mgonjwa aliyefariki baada ya Ramadhaan akiwa na deni

Swali: Ramadhaan iliyopita tarehe 21 baba yangu hakufunga kwa sababu ya maradhi na akafariki hospitalini tarehe 9 Shawwaal. Ni ipi hukumu?

Jibu: Ikiwa alikuwa na maradhi yasiyotarajiwa kupona basi alitakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini. Ikiwa ni maradhi yanayotarajiwa kupona lakini baada ya kutoka Ramadhaan maradhi yakamfisha – kama lilivyo wazi swali lako – hakuna kinachomlazimu. Kwa sababu kilichokuwa cha wajibu kwake ilikuwa ni kulipa lakini hata hivyo hakuweza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/122)
  • Imechapishwa: 09/06/2017