Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

15- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho azungumze [mambo ya] kheri au anyamaze; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu jirani yake; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake.”

Mgeni hupewa nini? Mgeni hupewa kile chenye kupatikana. Kwa msemo mwingine mgeni hupewa kitu ambacho mtu anailisha familia yake. Sio wajibu kwake kujikalifisha juu yake, kama mfano wa kumchinjia, kumpikia chakula kingi na mfano wa hayo. Lililo la wajibu ni kile alichojaaliwa na kinaweza kusitisha njaa ya mgeni huyu miongoni mwa chakula ambacho amezoea kula.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 246
  • Imechapishwa: 14/05/2020