Mfungaji kutumia kifaa cha kuvuta pumzi kinaharibu swawm?


Swali: Mfungaji kutumia kifaa cha kuvuta pumzi (inhaler) kinamfunguza?

Jibu: Kifaa hiki anachotumia hakifiki tumboni mwake. Kwa ajili hiyo tunasema hakuna neno kutumia kifaa hiki ilihali umefunga na wala hakikufunguzi. Kwa sababu ni kama tulivyosema tumboni hakuingii kitu. Ni kitu ambacho mtu anajipuliza nacho na kinaondoka. Hakiingizi kitu tumboni mpaka tuseme kuwa kinapelekea kufunguza. Kwa hivyo inajuzu kukitumia ilihali umefunga. Hakiharibu swawm yako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/209-210)
  • Imechapishwa: 09/06/2017