Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kula na kunywa kwa kusahau? Kipi mtu afanye akikumbuka wakati yuko anakula na anakunywa?

Jibu: Tumetangulia kusema kuwa mwenye kusahau haiharibiki funga yake ijapo atakula na kunywa sana. Muda wa kuwa amesahau swawm yake ni sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusahau ambapo akala au akanywa basi aikamilishe swawm yake. Kwani si vyengine Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[1]

Lakini anatakiwa kuacha kula na kunywa pale tu atapokumbuka. Tukikadiria kuwa tonge au kinywaji kiko mdomoni mwake, basi analazimika kutema. Kwa sababu hapo ule udhuru ambao Shari´ah imefanya ni kikwazo cha kufungua kitakuwa kimeondoka.

[1] al-Bukhaariy (1933) na Muslim (1155).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/275)
  • Imechapishwa: 01/05/2021