Mfungaji anatokwa na manii bila masababisho yoyote


Swali: Napenda kukujuza ya kwamba mimi natokwa na manii mchana wa Ramadhaan bila ya kuota kabisa, kumgusa mwanamke wala kujichukua sehemu ya siri. Je, kitendo hichi kinaathiri swawm yangu?

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivyoeleza kutokwa kwako na manii mchana wa Ramadhaan bila ya kuhisi matamanio yoyote hakuathiri swawm yako. Huhitajii kulipa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/279)
  • Imechapishwa: 11/06/2017