Mfungaji anasita “niendelee kufunga au nifungue”

Swali: Mfungaji akiweka nia ya kufungua kwa kukata anafungua?

Jibu: Ni jambo linalotambulika kwamba swawm imekusanya kati ya nia na kuacha ambapo mtu ananuia kwa funga yake kujikurubisha kwa Allaah na kuacha vifunguzi. Akiazimia kuikata basi swawm yake inaharibika. Lakini ikiwa ni katika Ramadhaan atalazimika kujizuia mpaka lizame jua. Kwa sababu kila mwenye kula katika Ramadhaan pasi na udhuru ni lazima kwake kujizuia na baadaye kulipa siku hiyo. Lakini ikiwa hakuazimia lakini alisita ni jambo ambalo wanachuoni wametofautiana.

1- Wako waliosema kuwa swawm yake inabatilika. Kwa sababu kutilia shaka kunapingana na kuazimia.

2- Wengine wakasema kuwa haibatiliki. Kwa sababu msingi ni kubaki kwa nia mpaka aazimie kuikata na kuindosha. Kwa mtazamo wangu haya ndio maoni yenye nguvu kutokana na kuwa kwake na nguvu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 467
  • Imechapishwa: 29/04/2020