Mfungaji amemwingilia mke wake usingizini

Swali: Ramadhaan ya mwaka 1396 nililala na mke wangu akiwa pembezoni na mimi. Sikuamka isipokuwa wakati kunaadhiniwa adhaana ya alfajiri. Lakini usingizi ukanishinda. Halafu nikaamka kabisa kama nimefunga ambapo nikamwingilia mke wangu usingizini kama kawaida yangu. Wakatiwa alfajiri nikaoga na kuswali alfajiri. Nimejuta sana kutokana na nilichokifanya. Ni kipi kinachonilazimu mimi na mke wangu pamoja na kujua kuwa hajui hukumu za mfungaji kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan pamoja vilevile na kujua kuwa baadaye ndipo alinikumbusha ambapo nikamuuliza ni kwa nini hakunikumbusha wakati wa jimaa au kabla yake. Akanambia kuwa hajui.

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivosema ambapo umemwingilia mke wako hali ya kusahau kuwa umefunga hulazimiki kulipa wala kutoa kafara. Kwa kuwa umesahau kwa kusahau. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusahau ilihali amefunga ambapo akala au akanywa basi atimize swawm yake. Hakika si mwengine ni Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[1]

Jimaa inachukua hukumu hiyo hiyo.

Kuhusu mwanamke lililo salama zaidi kwake yeye ni kulipa na kutoa kafara. Kwa sababu udhahiri kutokana na uliyoyataja ni kuwa ana elimu lakini hata hivyo alichukulia wepesi. Tunamuomba Allaah awasamehe wote.

Kafara ni kuacha mtumwa huru. Asipoweza afunge miezi miwili mfululizo. Asipoweza alishe masikini sitini. Kiwango chenyewe ni Swaa´ thelahini katika tende, mchele, ngano au chakula chenginecho anachowalisha familia yake. Kila masikini ampe nusu ya Swaa´.

[1] al-Bukhaariy (1933), Muslim (1155) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/306-307)
  • Imechapishwa: 14/06/2017