Swali 426: Mfungaji akisukutua kinywa au akapandisha maji puani ambapo yakaingia tumboni mwake kunamfunguza?

Jibu: Mfungaji akisukutua kinywa au akapandisha maji puani yakaingia tumboni mwake hakumfunguzi. Kwa sababu hakufanya kwa kukusudia. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ

”Hapana dhambi juu yenu katika yale mliyoyakosea, lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu.” (33:05)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 481
  • Imechapishwa: 29/04/2020