Swali: Kuna mtu ana ugonjwa wa kutokwatokwa hovyo na mkojo ambapo akataka kujikamua dhakari yake na matokeo yake akatokwa na manii. Ni lipi linalomuwajibikia?

Jibu: Lililo wajibu kwa huyu mfungaji ni yeye kuepuka kujikamua dhakari yake ikiwa anahisi matamanio. Kwa sababu inatambulika kuwa pindi matamanio yanapokuwa na nguvu mtu hushusha. Akiendelea kufanya hivo mpaka akatokwa na manii kwa matamanio basi anapata dhambi na swawm yake inaharibika. Katika hali hiyo analazimika kujizuia na kula na kunywa siku iliyobaki. Lakini akitokwa na manii bila ya matamanio swawm yake ni sahihi na wala halazimiki kulipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/237-238)
  • Imechapishwa: 12/06/2017