Mfungaji akiazimia kukata swawm inavunjika

Swali: Msafiri ambaye amefunga lakini akanuia kula kwa sababu safari ilimtia uzito. Lakini baada ya hapo akakamilisha swawm yake. Je, anazingatiwa ni mwenye kufuturu kwa nia pamoja na kwamba hakula na wala hakunywa?

Jibu: Akiazimia kukata nia anakuwa ni mwenye kufungua. Ama akiwa na mashaka; nile nisile; nina haja ya kula au sina; huyu ni mwenye mashaka na nia yake haikatiki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-18.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020