Mimi vitabu vyangu vimesoma Shaykh al-Albaaniy ambaye ni imamu wa Ahl-us-Sunnah katika zama hizi. Kadhalika ndugu yake Ibn Baaz. Yeye alikuwa hawezi kusoma. Lakini hata hivyo anachukua maneno ya wanachuoni wanaomfikishia khabari.

al-Albaaniy anasema nimesoma vitabu vyako na sikupata kosa hata moja na sikuona umetoka kwenye kitu hata kimoja ambacho tukoemo, akimaanisha mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hamtoshelezwi na ushuhuda huu au mnataka ushuhuda wa waongo na wenye kuzua! Huu ni ushuhuda wa mwanachuoni ambaye amebobea katika kujua Qur-aan na Sunnah na mfumo wa Salaf na kujua Bid´ah na upotevu. Akamshuhudia masikini huyu – yaani Shaykh Rabiy´ – ya kwamba hakuona kosa lolote. Sidai ya kwamba nimekingwa na makosa. Pengine kukawa kuna makosa na yakanipitikia. Lakini – himdi zote ni za Allaah – kudhihiri kwa kheri na haki juu ya vitabu hivi ndio ikawa mtu huyu akatoa ushuhuda huu.

Hivyo basi, yule anayetaka kheri asome vitabu hivi na anufaike navyo. Vitampambanulia kati ya haki na batili, Sunnah na Bid´ah. Na yule asiyetaka jengine isipokuwa kufuata kichwa mchunga wajinga na wapumbavu, njia za Shaytwaan ni nyingi. Yule anayetaka kuikoa nafsi yake, safina ya uokozi ni Qur-aan na Sunnah ambavyo tunalingania kwayo, mfumo wa Salaf tunaolingania, vitabu ambavyo vinaiweka wazi na kuisapoti na kuinusuru na kuitetea. Hii ndio njia ya uokozi. Njia ya maangamivu ni hizi ambazo zinawapiga vita Ahl-us-Sunnah, kuchafua mfumo wa Salaf, misingi yao, Salafiyyah kwa dhati yake na matendo yake. Hatukuona wakifanya chembe ya mambo haya kuwafanyia Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal. Mabalaa yote walonayo na shari wanayaelekeza katika mfumo wa Salaf na Salafiyyuun.

Pamoja na yote hayo, ole wako lau utasema kuwa huyu sio Salafiy. Sasa ikiwa wewe unaona kuwa Salafiyyah haina maana yoyote ni kwa nini unasema “mimi ni Salafiy” na ni kwa nini unakasirika mtu akikwambia kuwa “wewe sio Salafiy”? Ni kwa vile unaona kuwa haina maana yoyote. Waachie wenye nayo. Badala yake sema “mimi ni Tabliyghiy”, “mimi ni Ikhwaaniy”, “mimi ni Raafidhwiy” na kadhalika. Chukua madhehebu mengine kwa kuwa unaonelea kuwa Salafiyyah haina maana yoyote kwako.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2020