Haki ambayo haina shaka yoyote ndani yake ni yale waliokuwa wakifuat karne bora kisha wale waliowafuatia halafu wale waliowafuatia. Walikuwa wakionelea kuzipitisha Aayah za sifa kwa udhahiri wake na wala hawajikakami yale wasiyoyajua. Walikuwa hawakengeushi, hawafasiri kimakosa. Haya yanatambulika kupitia maneno yao, matendo yao na madhehebu yao jambo ambalo halina shaka yoyote wala hakuna mwenye kulipinga.

Wakati anapozuka mwanzilishi katika wakati wao basi walikuwa wakiwawekea wazi watu jambo lao na kuwabainishia kwamba yuko upotofuni. Walikuwa wakiyasema hayo wazi hadharani na kwenye mikusanyiko mikubwa. Walikuwa wakiwatahadharisha watu kutokamana na Bid´ah zake. Kwa mfano walifanya hivo wakati alipojitokeza Ma´bad al-Juhaniy na wafuasi wake ambao walikanusha Qadar. Matokeo yake wakamsambaratisha na wakawabainishia watu ubatilifu na upotevu wake ili watu watahadhari naye. Hakuna walioangamia isipokuwa wale ambao amepiga mihuri kwenye nyoyo zao na akaweka kizibo kwenye macho yao.

Hali hiyohiyo ndio waliokuwa nayo wale waliokuja baada yao; walikuwa wakiwabainishia watu ubatilifu wa madhehebu ya watu wapotevu. Waliendelea kufanya hivo mpaka ikawa mzushi ambaye amezusha katika sifa za Allaah hawezi kuonyesha Bid´ah yake. Walikuwa wanaificha kama ambavo mazanadiki walivokuwa wakificha ukafiri wao. Hivo ndivo wanavokuwa wazushi wengine wote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Aliy ash-Shawkaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tuhaf fiy Madhaahib-is-Salaf, uk. 17
  • Imechapishwa: 03/03/2019