Mfumo wa Ashaa´rah juu ya sifa za Allaah


Tambua kwamba watu wengi hii leo ni Ashaa´irah. Madhehebu yao inapokuja katika sifa za Mola (Subhaanahu wa Ta´ala) ni yenye kuafikiana na Mu´tazilah na Jahmiyyah.Wanathibitisha baadhi ya sifa tofauti na zengine.Wanathibitisha:

1- Uhai.

2- Elimu.

3- Uwezo.

4- Matakwa.

5- Kuona.

6-  Kusikia.

7- Maneno.

Sifa zengine zote mbali na hizi wanazikanusha kwa upindishaji ambao ni batili. Pamoja na kwamba wanaafikiana na Ahl-us-Sunnah katika kuthibitisha sifa ya maneno, uhakika wa mambo ni kwamba wanaikanusha. Kwa sababu maneno kwa mtazamo wao ni maana peke yake. Aidha wanasema kuwa herufi za Qur-aan zimeumbwa na kwamba Allaah hazungumzi kwa herufi wala sauti. Jahmiyyah wanasema kwamba hayo ndio ambayo pia wao wanasema pindi wanapodai kwamba Qur-aan imeumbwa, wanachokusudia ni herufi na sio ile maana.

Ahl-us-Sunnah wote wanasema kwamba maneno ya Allaah hayakuumbwa, kwamba Allaah amezungumza kwa Qur-aan kwa herufi na maana na kwamba Allaah (Subhaanah) anazungumza kwa suati inayosikika na yule Anayemtaka.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan Abaa Butwayn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Rasaa-il wal-Masaa-il an-Najdiyyah (2/176-177)
  • Imechapishwa: 14/03/2019