Swali: Nakuletea jarida hii ambayo inatawanywa mara kwa mara isemayo:

”Ndugu zangu waislamu wa kiume na waislamu wa kike! Kuna msichana mmoja wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 13 aliyekuwa mgonjwa maradhi makali ambaye mpaka madaktari wakashindwa kumtibu. Usiku mmoja maradhi yalimkuia makali na msichana huyu akalia mpaka usingizi ukamchukua. Usingizini mwake akamuona bibi Zaynab (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba aliweka mdomoni mwake matone. Wakati alipoamka kutoka usingizini mwake akajiona kuwa amekwishapona kabisa kutokamana na maradhi yake. Bibi Zaynab (Radhiya Allaahu ´anhaa) akamuomba aandike mapokezi haya mara kumi na tatu na pia ayaeneze kwa waislamu wa kiume na waislamu wa kike ili waweze kuona uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´aa)… ”

Ni lipi jukumu la walinzi wa usalama katika kuondosha mambo kama haya?

Jibu: Jarida hili ni batili. Yeyote mwenye kulipata ni lazima kulichoma moto. Ni lazima kumuadhibu yule mwenye kulieneza na akemewe juu ya jambo hilo. Hizi ni njama za shaytwaan. Hii ni ndoto ya ki-Shaytwaan. Malengo yake anataka kuwashughulisha watu kwa jambo hili na awalinganie kuchupa mpaka kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama Zaynab na wengineo kama wanavofanya Raafidhwah. Hii ni ndoto ya ki-Shaytwaan isiyokuwa na msingi wowote. Bali ni lazima kuipasua, kuitia moto na kuikemea.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3680/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%86%D8%B4%D8%B1%D8%A7%D8%AA-%D9%82%D8%B5%D8%B5-%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%81%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%AE%D9%8A%D8%A7%D9%84%D9%8A%D8%A9-%D9%88%D9%86%D8%AD%D9%88%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 05/03/2020