Swali: Je, inajuzu kwa mlinganizi kusema:

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa majina na sifa Zako kuu.”?

Je, du´aa hii huku ni kuiomba sifa?

Jibu: Nakuomba kwa majina mazuri kabisa na sifa Zako kuu, huku ni kutawassul kwa Allaah kwa majina na sifa Zako. Sio kuomba sifa. Ni kumuomba Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

”Allaah ana majina mazuri kabisa. Hivyo basi, muombeni kwayo. Waacheni wale wanaopotoa/haribu katika majina Yake. Watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.” (al-A´raaf 07:180)

Hiyo “kwa” (باء) ni Tawassul. Ni kama mfano wa:

“Kwa rehema Zako nakuomba msaada.”

Hii ni Hadiyth.

Swali: Ni upi mfano uliokatazwa wa kuomba sifa ya Allaah?

Jibu: Kama vile kusema “Ee uso wa Allaah!”, “Ee rehema za Allaah!” na mfano wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 77
  • Imechapishwa: 23/02/2019