Tunapowaambia watu kwamba unyoaji wa ndevu ni haramu huku sio kukazia au kuwa na msimamo mkali katika dini. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Punguzeni masharubu na refusheni ndevu.”

Tunapowaambia watu kwamba TV haina kheri ndani yake na kwamba ni lazima tuyasafishe majumba yetu kutokamana nayo sio kuwa na msimamo mkali. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Malaika hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa wala picha.”

Tukiwaamrisha wanawake zetu kuvaa Hijaab sio kuwa na msimamo mkali. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amesema katika Kitabu Chake kitukufu:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake [wote] wa Waumini – ya kwamba [nje ya nyumbani] wajiteremshie mavazi yao ya juu; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane [kuwa ni wanawake wa heshima] na wasiudhiwe. Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Tunaposema kwamba makaburi au makuba yaliyonyanyuliwa juu ya makaburi hayavunjwe sio kuwa na msimamo mkali. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha ´Aliy bin Abiy Twaalib asiache kaburi lolote lililonyanyuliwa isipokuwa alisawazishe wala picha isipokuwa aipasue. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kujenga juu ya makaburi na kuyaweka chokaa. Pindi sisi tunapomuigiza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah zetu hatuna msimamo mkali. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalini kama mlivyoniona ninaswali.”

Sisi hii leo tuna haki zaidi ya kusifiwa mapungufu kuliko kusifiwa kwamba tuna msimamo mkali. Hakika sisi tuna mapungufu. Ukweli wa mambo ni kwamba ni wapungufu na sio wenye msimamo mkali. Liko wapi jambo la kuamrisha mema na kukataza maovu?  Kadhalika katika mambo mengi sisi tunazingatiwa ni wenye kufanya mapungufu.

[1] 33:59

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 364-365
  • Imechapishwa: 13/10/2019