Mfano namna ambavyo al-Hajuuriy hana adabu kwa maimamu wa Ahl-us-Sunnah


Ndugu yetu Yahyaa al-Hajuuriy mara nyingi utamuona ni mwenye kuwakosoa maimamu waliotangulia katika darsa na vitabu vyake na mwenye papara ya kujishughulisha na kuwakosoa. Hutoona katika maneno yake kuwatafutia nyudhuru kama Ijtihaad za wanachuoni na mengineyo. Utamuona ni mwenye kutoa ibara zenye nguvu. Kwa mfano kanuni ya kimsingi iliyowekwa na Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) pale aliposema:

“Inatakiwa kuacha kupambanua nafasi ambayo inaweza kuleta maana nyingi kunateremka manzilah ya ujumla.”

Amesema kuhusu kanuni hiyo:

“Ikojolee.”

Vilevile amesema kuwa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab at-Tamiymiy ni mdhaifu katika elimu ya Hadiyth[1].

Kadhalika amesema kusoma katika “Fath-ul-Baariy” ni bora kuliko kusoma katika “Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah”. al-Haafidhw [Ibn Hajar] anataja dalili juu ya masuala. Kuhusu “Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah” wao hutoa tu ibara kama:

“Halali au haramu”

juu ya maoni yao bila ya kutaja dalili. Isitoshe “Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah” watu wamekuwa wanacheza nazo na wamekuwa wanazitumia kama hoja kama mfano wa vitabu vya ´Aliy al-Halabiy, Mashuur Hassan Salmaan na wengineo.

[1] Tazama https://www.youtube.com/watch?v=aXz3S0pvihg

  • Mhusika: Shaykh Abu ´Ammaar ´Aliy al-Hudhayfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://m-noor.com/showthread.php?p=33728
  • Imechapishwa: 12/02/2017