Mchumba anayepuuzia swalah ya al-Fajr


Swali: Kuna mwanaume amekuja kutaka kumchumbia msichana wangu na ikanibainikia ya kwamba haswali al-Fajr isipokuwa pale anapoamka kutoka usingizi baada ya jua kuchomoza. Nifanye nini kabla ya ndoa?

Jibu: Usimuozeshe mpaka atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na aamke kuswali swalah ya al-Fajr pamoja na waislamu wenzake. Atapotubia na kunyooka na akaswali pamoja na waislamu wenzake hapo ni sawa kumuozesha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (60) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16548
  • Imechapishwa: 16/09/2017